728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 12, 2017

    Mashabiki wa Simba SC lawamani kwa uharibifu wa Uwanja wa CCM Kirumba


    Mwandishi Wetu,Mwanza.

    Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba, kupitia Meneja wa Uwanja Ndugu Steven E. Shija unapenda kutoa taarifa za uharibifu wa Uwanja.

    Mechi iliyochezwa Tarehe 10.04.2017, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kati ya Mbao FC Vs Simba SC umesababisha uharibifu Mkubwa kwenye Maeneo ya kuingilia Wachezaji, Waamuzi na Geti Namba 4 ambapo walikuwa wamekaa Mashabiki wa Simba

    Uharibifu huo umetokana na Mashabiki wa Timu ya Simba SC kupanda Juu ya maeneo ya Kivuli yaliyojengwa kwenye maeneo yaliyotajwa ( Vyumba vya Kubadirishia Nguo kwa wachezaji, Waamuzi na Geti namba Nne), uharibifu huo umepelekea kushindwa kufunga Milango ya Mbele ambapo ni hatari kwa usalama wa maeneo hayo muhimu


    Hivyo uongozi wa Uwanja umeishazitaarifu Mamlaka husika ili zichukue hatua kwa Wanaohusika ili kuhakikisha eneo hilo linatengenezwa mapema kabla ya Mechi ya Toto African Vs Simba SC Tarehe 15.04.2017 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mashabiki wa Simba SC lawamani kwa uharibifu wa Uwanja wa CCM Kirumba Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top