728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 12, 2017

    Hatimaye Neymar afungiwa Hispania


    Barcelona,Hispania.

    SASA ni rasmi kuwa Barcelona itamkosa Neymar kwenye mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid Aprili 23 hii ni baada ya staa huyo wa Brazil kukumbana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi ya La Liga kwa utovu wa nidhamu.

    Kufungiwa kwa Neymar kunatokana na matukio mawili yasiyo ya kiungwana aliyoyafanya Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa La Liga uliomalizika kwa klabu yake ya Barcelona kufungwa mabao 2-0 na Malaga huko LaRosaled

    Katika mchezo huo Neymar Neymar alitolewa uwanjani katika dakika ya 60 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.Kadi ya kwanza ya njano ilitokana na kuzuia upigwaji wa faulo kwa kwenda kufunga kamba za viatu mbele ya mpira huku kadi ya pili ikitokana na kumchezea madhambi Diego Llorente.Kosa hilo adhabu yake ni kukosa mchezo mmoja.

    Lakini wakati anaelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo,Neymar alifanya utovu mwingine wa nidhamu baada ya kunaswa akimkejeli mwamuzi msaidizi kwa kumpigia makofi tukio ambalo ni kinyume cha taratibu na adhabu yake huwa ni kufungiwa.Ambapo Neymar amefungia michezo miwili zaidi na jumla kuwa amefungiwa michezo mitatu kwa makosa hayo mawili.

    Sasa hii ina maana kwamba Neymar ataukosa mchezo wa wikendi ijayo dhidi ya Real Sociedad kisha michezo dhidi ya Real Madrid na Osasuna.

    Wakati huohuo taarifa kutoka ESPN FC zinasema Barcelona imesema itakata rufaa kupinga adhabu hiyo kwa madai kuwa ni kali mno hasa kwa mchezaji ambaye ndiyo mara yake ya kwanza kutolewa dimbani kwa utovu wa nidhamu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hatimaye Neymar afungiwa Hispania Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top