728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 12, 2017

    Rufaa ya Simba SC kwa Fakhi yageuka vita ya Salum Mkemi na Haji Manara



    Mwandishi Wetu,Dar Es Salaam.

    Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga imeitaka bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara kuacha kuipa pointi za mezani timu ya Simba kufuatia rufaa waliyomkatia beki wa Kagera Sugar Mohammed Fakhi aliyetajwa kuwa na kadi tatu za njano. Kikao hicho kilifanyika jana ambapo kwa pamoja wametoa tamko kwa kupinga rufaa hiyo kwakuwa ina atharikwa Yanga katika kutetea ubingwa wake.

    Mjumbe wa Kamati hiyo Salum Mkemi amewaambia waandishi wa Habari kuwa tayari wamepeleka malalamiko kwa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ili kuchunguza barua pepe zilizotumwa na mwamuzi wa mchezo huo kwenda kwa Kamati. Mkemi alisema kwa mujibu wa kanuni za ligi mwamuzi anapaswa kutuma ripoti ya mechi ndani ya masaa 48 na akishindwa anapaswa kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi wanaotakiwa kuchezesha ligi.

    “Kamati imetoa tamko kwa bodi ya ligi kutowapa pointi Simba kwakuwa jambo hilo litakuwa ni sawa na kuwabeba Simba waziwazi kitu ambacho hatutakubali kitokee,” alisema Mkemi.

    Mjumbe huyo aliongeza: “hatuna shida na ushindi wa Simba wa uwanjani kama walivyoshinda jana dhidi ya Mbao FC wakitoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2, mbona hakuna aliyelalamika?, ila kwa hili hatutakubali litokee.”

    MAJIBU YA HAJI MANARA 

    Leo mchana huu kunatembea taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria.  Taarifa hiyo ya Yanga iliomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeoongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani, pia taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano. 

                           

    Klabu ya Simba inawaambia viongozi wa Yanga wanayo mambo ya msingi ya kuwashughulisha, ikiwepo kutafuta mishahara ya wachezaji wao iliokwama kwa miezi kadhaa kama inavyoripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari,pia waangalie namna bora ya kuurejeshea hadhi uwanja wake wa mazoezi wa Kaunda ili upate kuchezeka tena na sio ulivyo hivi sasa,ambapo umegeuka kama bwawa la kufugia kambale,,ni kushangazwwa kulikochupa mpaka kufuatilia rufani isiyowahusu,Hii ni rufani ya Simba dhidi ya Kagera sio wao Yanga.

    Tunaamini bodi haitafanya maamuzi kwa shinikizo la yoyote yule,na hatutarajii kuona porojo walizozisema leo zitaondoa ukweli uliopo mezani kwao ambao klabu yetu imeuwasilisha.Mwisho niwaombe washabiki wetu watulie na waiachie bodi ifanye maamuzi yake ambayo tunaamini yatatoa haki kwa anayestahili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Rufaa ya Simba SC kwa Fakhi yageuka vita ya Salum Mkemi na Haji Manara Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top