728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 13, 2017

    Kipa namba moja wa wapinzani wa Yanga,MC Alger jela miezi sita


    Algers,Algeria.

    KIPA namba moja wa MC Alger ya Algeria,ambao ni wapinzani wa Yanga kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika,Faouzi Chaouchi amehukumiwa kwenda jela miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia kwa makonde afisa mmoja wa polisi. 

    Chaouchi, 32,ambaye Jumamosi iliyopita aliibania Yanga kupata mabao ya kutosha baada ya kuokoa michomo ya hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni kwake, amekumbana na adhabu hiyo juzi Jumanne katika shauri lake lililokuwa likisikilizwa kwenye mahakama ya wilaya ya Bir Mourad Rais.Hata hivyo kifungo hicho kimesimamishwa mpaka hapo baadae.

    Aprili 7 mwaka huu Chaouchi mwenye rekodi mbaya ya utovu wa nidhamu alifikishwa mahakamani baada ya kumshambulia kwa makonde afisa wa polisi aliyekuwa amepewa jukumu la kuwafanyia ukaguzi wachezaji kabla ya kuingia uwanjani.


    Katika utetezi wake Chaouchi alikana kumshambulia afisa huyo wa polisi na kusema kuwa alimsukuma akipinga kufanyiwa ukaguzi mwilini mwake kabla ya kuingia uwanjani.

    Televisheni binafsi ya Echorouk imeripotiwa kuwa mbali ya adhabu hiyo ya kifungo pia Chaouchi ameamuliwa kulipa faini ya Dinari za Algeria,50,000 ambazo ni sawa na Dola za Marekani 450.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kipa namba moja wa wapinzani wa Yanga,MC Alger jela miezi sita Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top