Faridi Miraji,Dar Es Salaam.
Baada ya Sarakasi za hapa na pale ..hatimaye muda unaamua sasa.Kamati ya Saa 72 inatarajia kukutana leo Saa 9:00 Alasiri kumalizia kujadili Malalamiko ya Simba SC wakidai kwenye mechi yao waliyofungwa 2-1 na Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba Aprili 2 Mwaka huu, Kagera Sugar 'Wanasupa Nkurukumbi' walimchezesha Mlinzi wao wa kati Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano kinyume na kanuni za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Simba wanalalamika kuwa Fakhi alipata kadi kwenye mechi za Timu yake dhidi ya Mbeya City, African Lyon na Majimaji FC.Kagera Sugar wanakubali kadi mbili, ya Mbeya City na Majimaji FC, lakini ya African Lyon hawaitambui. Kutokana na hilo kamati iliahirisha sakata hilo ili kujiridhisha kwa kupitia Ripoti za michezo yote inayotajwa kabla ya kuamua.
Taarifa za awali zinadai kwenye mechi hiyo ya Africa Lyon, Fakhi alioneshwa kadi ya njano Dakika ya 74' na ndio ilikuwa kadi pekee katika mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment