728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 13, 2017

    Nisipowapeleka kombe la dunia,nitaondoka zangu


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    AHADI!!MJERUMANI,Gernot Rohr ameahidi kuwa atajiuzulu kuifundisha Nigeria ikiwa atashindwa kuipa miamba hiyo ya Afrika Magharibi tiketi ya kushiriki kombe la dunia la mwaka 2018 litakakofanyika nchini Urusi.

    Rohr amepata ushujaa wa kutoa ahadi hiyo nzito hii ni baada ya hivi karibuni kuzianza vyema mbio za kuwania tiketi ya kombe la dunia kwa kuzifunga Zambia na Algeria katika michezo ya awali na kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi B lenye timu nne wakiwemo mabingwa wa Afrika,Cameroon ambao watakaovaana nao kwenye miezi Agosti na Septemba.

    Rohr mwenye umri wa miaka 63 amekiri kuwa anawaona Cameroon kuwa ndiyo wapinzani wao wakubwa kwenye kundi lao la B lakini amesema hiyo bado haitafanya asijiuzulu ikiwa Nigeria itashindwa kufuzu kombe la dunia. 

    Kama hatutashinda tiketi ya kombe la dunia,nitasema kwaheri.Nitachukua kila kitu changu na kuondoka.

    Tuna mchezo ngumu dhidi ya Cameroon.Ni changamoto ambayo niko tayari kukabiliana nayo na nikishindwa nitaondoka zangu.

    Rohr alianza kuifundisha Nigeria Agosti 2016 akichukua mikoba ya mzawa, Sunday Oliseh aliyejiuzulu baada ya kuhudumu kwa muda mfupi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nisipowapeleka kombe la dunia,nitaondoka zangu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top