728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 13, 2017

    Ligi kuu bara kuendelea tena leo,ratiba nzima ya wikendi iko hapa


    Mbeya,Tanzania.

    LIGI kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo mmoja kuchezwa huko mkoani Mbeya ambapo wenyeji Mbeya City watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine kuwaalika African Lyon kuanzia saa 10:00 jioni.

    Timu hizo zinaingia uwanjani zikitofautiana kwa nafasi nne.Mbeya City iko nafasi ya sita ikiwa na pointi zake 32 baada ya kucheza michezo 27.African Lyon iko nafasi ya kumi ikiwa na pointi zake 30 baada ya kucheza michezo 26.

    Aidha katika mchezo huo Mbeya City itamkosa wingi wake, Mrisho Ngassa anayesumbuliwa na majeruhi.

    Ligi itaendele Jumamosi kwa michezo minne, Stand United wakiwa wenyeji wa
    Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Kambarage,Shinyanga na Toto Africans
    wakiikaribisha Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

    Mechi nyingine za Jumamosi, Majimaji ya Songea itaifuata Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani -mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana wakati JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

    Kwa mujibu wa ratiba,Jumapili Mbao watacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza huku Mwadui wakiwa wenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Mwadui,Shinyanga.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ligi kuu bara kuendelea tena leo,ratiba nzima ya wikendi iko hapa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top