728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 06, 2017

    Arsenal yairejesha Man United nafasi ya sita England


    London, England.

    ARSENAL imefanikiwa kuirejesha Manchester United mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka ya England baada ya usiku huu kuifunga West Ham United kwa jumla ya mabao 3-0 nyumbani Emirates.

    Arsenal ambayo ilikuwa haijaonja radha ya ushindi kwenye ligi kuu tangu Februari 11 imejipatia mabao hayo katika kipindi cha pili cha mchezo kupitia kwa Mesut Ozil 58', Theo Walcott 68' na Olivier Giroud 83'.Kipindi cha kwanza hakikushuhudia bao.

    Ushindi huo umeifanya Arsenal ifikishe pointi 54 na kushika nafasi ya tano ambayo hapo awali ilikuwa inashikwa na Manchester United ambayo sasa imeporomoka mpaka nafasi ya sita kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Arsenal yairejesha Man United nafasi ya sita England Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top