Abuja,Nigeria.
MKENYA Victor Wanyama ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari kwa wachezaji wa Afrika wanaocheza ligi kuu nchini England.
Wanyama,24,anayechezea Tottenham ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda winga wa Chelsea na Nigeria Victor Moses na kiungo wa Manchester City na Ivory Coast Yaya Toure.
Tuzo hiyo inayotolewa na New African Soccer imekuja baada ya Wanyama kuwa katika kiwango bora cha uchezaji kwa mwezi Januari ambapo aliiwezesha Tottenham kufanya vizuri kwenye michezo yake mingi.
0 comments:
Post a Comment