728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 15, 2017

    Wanane wapenya mchujo wa kuwania nafasi ya kuinoa Amavubi,wamo Samson Siasia na Georges Leekens.

    Kigali,Rwanda.

    JUMLA ya makocha wannane kutoka nje na ndani ya Afrika wameripotiwa kupenya kwenye mchujo unaoendeshwa na chama cha soka cha Rwanda (Ferwafa) ili kumpata kocha atakayeinoa Amavubi baada ya Muireland,Johnny McKinstry kutimuliwa kibarua hicho mwezi Augusti mwaka jana.

    Mnigeria Samson Siasia ni miongoni mwa makocha hao wanane waliopenya mchujo huo wa kumrithi McKinstry.

    Mwingine ni Mbelgiji Georges Leekens,ambaye ni hivi karibuni tu amejiuzulu kuifundisha Algeria baada ya Mbweha hao wa jangwani kuondolewa kwenye makundi ya michuano ya AFCON huko Gabon.

    Wengine ni Peter Butler anayeinoa Botswana.Raoul Savoy,Jose Rui Lopes Aguas,Antoine Hey na Winfried Schafer.

    Rais wa Ferwafa,Vincent Degaule Nzamwita,amesema wanalifanya zoezi hilo kwa umakini mkubwa kwani wanataka kuteua kocha atakayewapeleka mbali zaidi.

    Orodha kamili ya makocha waliopenya mchujo iko kama ifuatavyo:

    1. Antoine Hey (Germany)
    2. Georges Leekens (Belgium)
    3. Jose Rui Lopes Aguas (Portugal)
    4. Paul Put (Belgium)
    5. Peter James Butler (England)
    6. Winfried Schafer (Germany)
    7. Raoul Savoy (Switzerland)
    8. Samson Siasia (Nigeria)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wanane wapenya mchujo wa kuwania nafasi ya kuinoa Amavubi,wamo Samson Siasia na Georges Leekens. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top