Manchester, England
PIGO KUBWA:Gabriel Jesus ni kama ametibua hivi hesabu za ubingwa Manchester City hii ni baada ya kuripotiwa kuwa amechagua kufanyiwa upasuaji (kupigwa kisu) ili kutibu mfupa uliovunjika kwenye mguu wake wa kulia.
Juzi Jumatatu Gabriel,19, alishindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutolewa katika dakika ya 15 na nafasi yake kuchukuliwa na Sergio Aguero.Gabriel alivunjika baada ya kutua vibaya wakati akijaribu kumiliki mpira katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bournemouth huko Vitality.
Habari zinasema Gabriel aliambiwa na madaktari wa Manchester City achague kati ya kufanyiwa upasuaji ama afanyiwe matibabu ambayo kwa lugha ya kitaalamu yanajulikana kama physiotherapy.
Matibabu ambayo hayahitaji upasuaji na hufanya jeraha lipone ndani ya muda mfupi lakini athari yake ni kwamba jeraha hilo huweza kumrudia tena muhusika na ndipo hapo Gabriel alipoamua kuchagua upasuaji ambao utamweka nje ya dimba kwa kipindi cha kati ya miezi miwili mpaka mitatu mpaka kupona.
Hii ina maana kwamba sasa Manchester City itakuwa ikimtegemea zaidi Aguero kuhakikisha inaipiku Chelsea kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu England.
0 comments:
Post a Comment