728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 15, 2017

    Kiduku champonza Asamoah Gyan Uarabuni.

    Ahli,Qatar

    MAKUBWA!!Nahodha wa Ghana,Asamoah Gyan ameunza vibaya mwezi Februari baada ya chama cha soka cha nchini Qatar kumlima faini kwa kosa la kunyoa kiduku.

    Gyan,31,anayeichezea Al- Ahli kwa mkopo akitokea Shanghai SIPG ya China amelimwa faini hiyo ambayo hata hivyo haijatajwa ni kiasi gani.

    Mbali ya Gyan, wachezaji wengine zaidi ya 40 nao wamelimwa faini kutoka na taifa hilo la Kiarabu lenye imani kali ya dini ya kiislamu kupiga marufuku unyoaji wa mitindo ya ajabu ajabu inayofahanika kama ‘Qaza'.Mitindo isiyo na maadili ikiwemo kiduku.

    Kiduku ni unyoa wa nywele ambapo mnyoaji hunyoa nywele za pembeni na kuacha nywele nyingi kidogo juu.

    Ikumbukwe mwaka 2012 kipa wa Saudi Arabia, Waleed Abdullah aliamuriwa na mwamuzi kunyoa nywele zake kabla ya kuruhusiwa kuingia uwanjani kuichezea klabu yake ya Al Shabab.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kiduku champonza Asamoah Gyan Uarabuni. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top