Dar Es Salaam,Tanzania.
Mchezo
wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na
Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao
ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.
Nsulumbi
atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa
Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone
Lucas Nhlapo.
Mchezo
huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans
walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo
ambayo ni Februari 18, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment