Munich, Ujerumami.
Bayern Munich imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya Jumatano usiku kuisasambua Arsenal kwa mabao 5-1 nyumbani Allianz Arena katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano.
Arjen Robben ndiye aliyeanza kuifunga Bayern Munich bao la kwanza katika dakika ya 11 na kufuatiwa na mabao ya Robert Lewandowski katika dakika ya 53,Thiago Alcantara katika dakika za 56, 63 na Thomas Muller katika dakika ya 88.
Bao pekee la Arsenal katika mchezo huo limefungwa na Alexis Sanchez katika dakika ya 30 baada ya kuuwahi mkwaju wake wa penati uliookolewa na Manuel Neuter na kufunga.
Mkwaju huo wa penati ulipatikana baada ya mlinzi Laurent Koscielny kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la boksi na Robert Lewandowski.
Katika mchezo mwingine Real Madrid ikiwa nyumbani Santiago Bernabeu imeifunga Napoli mabao 3-1 kupitia kwa Toni Kroos Karim Benzema na Casemiro Bao la Napoli limefungwa na Lorenzo Insigne.
0 comments:
Post a Comment