Na Faridi Miraji
Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kusimama kwa muda wa mwezi mzima wa Machi kupisha michuano ya mbalimbali mwezi huo. Michuano hio ni pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam, Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho Afrika, kalenda ya FIFA ya mechi za kirafiki pamoja na michuano ya Kufuzu AFCON 2019.
Mechi za raundi ya 24 zitachezwa kati ya 4-5 Machi wakati zile za raundi ya 25 zitachezwa kati ya 02-4 Aprili. Baada ya mechi za raundi 24, kutakuwa na mechi za awali za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kati ya tarehe 10-12 Machi. Pia kutakuwa na baadhi ya mechi za Kombe la shirikisho Azam kwa baadhi ya timu.
Kati ya tarehe 17-19 Machi kutakuwa na mechi za marudiano ya Ligi ya Mabingwa, Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mechi za robo fainali za Kombe la Azam.
Baada ya hapo za kirafiki za kimataifa zinachukua mkondo katika kalenda ya FIFA inayoangukia kati ya Machi 20-28 ikijumuisha mechi za awali za kufuzu CHAN 2018 na AFCON 2019.
Kusimama huko sio jambo jipya kwa vilabu kwani ratiba iliyotolewa na TFF ilionesha hivyo tangu mwanzo mwa msimu.
0 comments:
Post a Comment