728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 13, 2017

    Barcelona yaruhusiwa kufanya usajili kuziba pengo la majeruhi Alex Vidal


    Barcelona,Hispania.

    Barcelona iko huru kusajili mchezaji wapya kwa ajili ya kuziba pengo la beki wake wa kulia aliye majeruhi,Aleix Vidal.Hii ni kwa mujibu wa sheria za soka za nchini Hispania.

    Juzi Jumamosi ,Vidal,27, aliumia vibaya kifundo chake cha mguu wa kulia katika ushindi wa Barcelona wa mabao 6-0 dhidi ya Alaves na imeripotiwa kuwa atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitano.

    Kuumia kwa Vidal siku ya Jumamosi kumeifanya Barcelona ibaki na Sergi Roberto pekee katika nafasi ya beki wa kulia ingawa siyo nafasi yake halisi. 

    Lakini sheria za soka za nchi ya Hispania zinasema kuwa klabu inapokumbwa na tatizo la majeruhi hasa yale ya muda mrefu basi itaruhusiwa kusajili wachezaji wapya hata kama dirisha la usajili litakuwa tayari limefungwa.

     Sifa za mchezaji kusajiliwa

    a) Mchezaji anapaswa kuwa ni raia wa Hispania ama awe ni mchezaji huru (asiye na timu).

    b) Atacheza michezo ya ndani ya Hispania pekee ambayo ni La Liga na Copa del Rey.

    Wakati huohuo ripoti kutoka nchini Hispania zinasema kocha wa Barcelona,Luis Enrique hafikirii kufanya usajili wowote katika kipindi hiki na badala yake atamtumia beki wa kikosi B cha Barcelona,Nili Perdomo kuziba pengo la Vidal.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Barcelona yaruhusiwa kufanya usajili kuziba pengo la majeruhi Alex Vidal Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top