Bournemouth,England.
MANCHESTER CITY sasa imechupa mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu England baada ya usiku huu ikiwa ugenini dimbani Vitality kuwafunga wenyeji wao Bournemouth kwa mabao 2-0.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi,Neil Swarbrick kutoka Lancashire na kushuhudiwa na watazamaji 11,129 ilishuhudiwa Manchester City ikipata bao lake la kwanza kupitia kwa Raheem Sterling katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Manchester City ilipata bao lake la pili katika dakika ya 69 ya kipindi cha pili baada ya mlinzi wa Bournemouth Tyrone Mings kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mkwaju wa Sergio Aguero aliyekuwa ameingia uwanjani kuchukua nafasi ya Gabriel Jesus aliyekuwa ameumia.
Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa bao la Bournemouth lililofungwa na Joshua King likikataliwa na mwamuzi,Neil Swarbrick kwa madai kwamba mfungaji alimvuta shati John Stones wa Manchester City kabla ya kufunga.
Sasa ushindi huo umeifanya Manchester City kufikisha pointi 52,pointi nane nyuma ya vinara Chelsea wenye pointi 60 katika michezo 25.Timu zote zimecheza michezo sawa.
Vikosi
AFC Bournemouth (4-1-4-1): Boruc;Smith, Francis (Mings, 22), Cook, Daniels;Surman; Ibe, Wilshere (Afobe, 45), Arter,Fraser; King.
Manchester City (4-3-3): Caballero;Sagna, Stones, Kolarov, Fernandinho; De Bruyne, Toure, Silva; Sterling, Gabriel (Aguero, 14), Sane.
0 comments:
Post a Comment