728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, February 14, 2017

    TP Mazembe yapata kocha mpya

    Lubumbashi,DR Congo.

    MIAMBA wa DR Congo,TP Mazembe wamemtangaza Mfaransa,Thierry Froger kuwa kocha wao mkuu mpya.

    Thierry mwenye umri wa miaka 53 sasa jana Jumatatu alisaini mkataba wa miezi kumi utakaomalizika Disemba 31,2017.

    Thierry anachukua nafasi ya Mfaransa mwenzie Hubert Velud aliyetimkia Etoile Du Sahel ya Tunisia mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuisaidia TP Mazembe kutwaa kombe la shirikisho Afrika na kombe la ligi ya DR Congo.

    Kocha huyo, beki wa zamani wa Lille,Le Mans na Genoble siyo mgeni na soka la Afrika kwani alishawahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Togo kati ya mwaka 2010 na 2011.

    Majukumu ya Thierry ndani TP Mazembe yataanza wikendi hii kwenye mchezo wa kuwania ubingwa wa CAF Super Cup ambapo miamba hiyo ya DR Congo itavaana na Mamemlodi Sundowns siku ya Jumamosi Februari 18, 2017 huko Pretoria,Afrika Kusini.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TP Mazembe yapata kocha mpya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top