728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 13, 2017

    Kumbe Pogba ni Arsenal damu

    Florentin Pogba


    Saint Etienne,Ufaransa.

    STAA wa Saint Etienne, Florentin Pogba,ambaye ni kaka mkubwa wa kiungo wa Manchester United,Paul Pogba,amefichua siri kwamba yeye ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal inayofundishwa na Mfaransa Arsene Wenger.

    Pogba mwenye umri wa miaka 26 sasa na tegemeo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Guinea amefichua siri hiyo hivi karibuni wakati akifanya mahojiano na gazeti la The Guardian na kudokeza kuwa amekuwa akiifuatilia Arsenal tangu msimu wa 2003/04 hasa pale ilichocheza msimu mzima bila kufungwa.




    Pogba ameongeza kuwa kivutio chake kikubwa kwenye kile kikosi cha Arsenal kilikuwa ni Wafaransa Patrick Vieira, Robert Pires na Thierry Henry ambao wakati huo walikuwa moto mkali ndani ya kikosi hicho.

    “Arsenal ni klabu ya moyo wangu.Nimekuwa nikiishabikia tangu wakati wa kile kikosi cha Invincibles kilichocheza msimu mzima bila kufungwa.Amesema Florentin.

    Hajawahi kuitazama live (Moja kwa Moja) Arsenal ikicheza!!

    "Tatizo la kuwa mchezaji wa kulipwa ni kuwa haupati muda mwingi wa kutazama timu nyingine zikicheza,hivyo sijawahi kwenda Emirates kuitazama Arsenal ikicheza.Natumaini siku moja itawezekana".

    Pogba uso kwa uso na Pogba!!

    Februari 22 mwaka huu Florentin na Paul Pogba watakuwa kwenye vikosi tofauti pale vikosi vyao vitakapoumana kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora ya michuano ya Europa Ligi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kumbe Pogba ni Arsenal damu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top