Na Faridi Miraji.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo miwili tu.
Michezo ya kesho kwa mujibu wa Ratiba ya VPL ni kati ya Ndanda FC itakayoikaribisha Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Kagera Sugar ya Kagera itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi nyingine zitachezwa Februari 17, 18 na 19 kwa mujibu wa Ratiba .
0 comments:
Post a Comment