Na Faridi Miraji
Raundi ya Sita ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup – 2016/17, itaanza Februari 16, 2017 badala ya Februari 24, mwaka huu.
Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja kabla ya kuendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaopigwa saa 1.00 jioni.
Michezo hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini
0 comments:
Post a Comment