Paris,Ufaransa.
Paris Saint-Germain imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu baada ya usiku huu kuichanachana Barcelona mabao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliochezwa huko Parc des Princes,Paris.
Nyota katika mchezo huo uliotawaliwa na wenyeji kwa kiwango kikubwa na Paris Saint-Germain alikuwa ni Muargentina, Angel Di Maria,29, aliyefunga mabao mawili katika siku ambayo pia alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa.
Angel Di Maria alianza kuifungia bao la kuongoza Paris Saint-Germain katika dakika ya 18 kwa mpira wa adhabu huku la pili akifunga katika dakika ya 55 kwa mkwaju mkali wa mbali.
Mabao mengine ya Paris Saint-Germain yamefungwa na Julian Draxler katika dakika ya 40 na Edinson Cavani katika dakika ya 71. Cavani pia alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa.Ametimiza miaka 30.
Ikiwa Paris Saint-Germain itafikiwa kuing'oa Barcelona katika hatua ya 16 bora basi itakuwa imepoza machungu ya kuondolewa kwenye hatua za robo fainali za mwaka 2013 na 2015.
0 comments:
Post a Comment