Benfica,Ureno.
BENFICA imeendeleza rekodi yake nzuri ya kutoruhusu bao lolote katika uwanja wake wa nyumbani wa Estadio da Luz mpaka kufikia dakika 383 baada ya Jumanne Usiku kuichapa Borussia Dortmund kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliochezwa huko Benfica,Ureno.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa katika dakika ya 48 na Mgiriki Kostas
Mitroglou baaada ya kupokea pasi safi ya kichwa kutoka kwa beki mkongwe wa Brazil,Luisao aliyekuwa anacheza mchezo wake wa 500 akiwa na Benfica.Hilo ni bao la 13 kwa Mitroglou katika michezo 13 iliyopita.
Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa nyota wa Gabon,Pierre Emerick Aubameyang akiikosesha bao la kusawazisha Borussia Dortmund katika dakika ya 58 baada ya mkwaju wake wa penati kupangulia na kipa wa Benfica,Ederson,hali iliyomlazimu mwalimu Thomas Tuschel kumtoa. katika dakika ya 62 na nafai yake kuchukuliwa na Schurrrle.
Timu hizo zitarudiana Machi 8,2017 na mshindi itafuzu robo fainali.
0 comments:
Post a Comment