Burnley,England.
WAMEBANA!!Hesabu za Chelsea kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu England kwa tofauti ya pointi nyingi kuliko timu nyingine za ligi hiyo zimekwama jioni hii baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Burnley huko Turf Moor.
Chelsea ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Pedro Rodriguez aliyefunga katika dakika ya 7 akimalizia Kazi safi ya Victor Moses.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Burnley ambao walikuja juu na kuibana vyema Chelsea na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Robbie Brady aliyefunga kwa mpira wa adhabu (Free- Kick) katika dakika ya 24 ya mchezo.
Aidha katika mchezo huo ulioshuhudiwa na watazamaji 21,744 ilishuhudiwa mwamuzi Kevin Friend akitoa kadi nne za njano.Tatu kwa Burnley na moja kwa Chelsea.
Sare hiyo imeifanya Chelsea ifikishe pointi 60 na kuendelea kukalia kiti cha uongozi.Burnley iko nafasi ya 12 na pointi zake 30.
0 comments:
Post a Comment