Cagliari,Italia.
JUVENTUS imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ya Seria A na sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba na wanaoshika nafasi ya pili AS Roma baada ya Jumapili Usiku kuibamiza Cagliari kwa mabao 2-0 ugenini huko Ezio Scida.
Mabao yote ya Juventus katika mchezo huo uliopigwa usiku mnene yamefungwa na mchezaji ghali zaidi Italia Muargentina Gonzalo Higuain "El Pipita" katika dakika za 37 na 47 shukrani kwa pasi safi za kiungo Claudio Marchisio na mshambuliaji Paulo Dybala.Sasa Higuain amefikisha mabao 18 Seria A.
Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa Cagliari ikimaliza na wachezaji 10 baada mlinzi wake Nicolo
Barella kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 67 kwa kumfanyia madhambi Miralem Pjanic.
Katika michezo ya mapema Roma ikiwa ugenini imeifunga Crotone 2-0 shukrani kwa mabao ya Radja Nainggolan na Edin Dzeko.
Inter Milan imejisogeza mpaka nafasi ya nne baada ya kuichapa Empoli 2-0 kwa mabao ya Eder na Antonio Candreva.Atalanta imeichapa Palermo 3-1 huku Pescara ikilala kwa mabao 5-3 kutoka kwa Torino.
0 comments:
Post a Comment