728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 04, 2016

    MKWASA AMPAKA CANAVARRO KWA KUKOSA UZALENDO

    Dar es salaam,Tanzania.

    KOCHA wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Charles Mkwasa ametoa la moyoni na kudai kuwa nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Canavarro’ sio mzalendo.

    Mkwasa aliyasema hayo jana wakati Stars ikiwa leo inashuka dimbani kucheza na Misri katika mchezo wa
    kuwania kufuzu kucheza michuano ya Mataifa ya African, Gabon mwakani.

    Mkwasa alimuita Canavarro siku chache zilizopita kwenye kikosi cha Stars kinachocheza leo, ili kuziba
    pengo la Kelvin Yondani ambaye anakabiliwa na adhabu ya kadi mbili za njano hivyo analazimika kukosa mchezo wa leo.

    Hata hivyo, Canavarro aliitolea nje ofa hiyo ya Mkwasa, kitendo ambacho kimeonesha kumkera,ambapo alisema hawezi kumlazimisha mbuzi kunywa maji.

    “Canavarro hana uzalendo kwa hiyo siwezi kumlazimisha ni kama uvute mbuzi kamba umpeleke mtoni kunywa maji akagoma, kwa hiyo muacheni na mambo yake,”alisema.

    Mapema mwaka huu, Canavarro alitangaza kustaafu soka la kimataifa kwa kutoichezea Stars baada ya kuvuliwa kitambaa cha unahodha na kukabidhiwa Mbwana Samatta. Baada ya beki mwingine Aggrey Morris ambaye alitangaza kustaafu

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MKWASA AMPAKA CANAVARRO KWA KUKOSA UZALENDO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top