728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 04, 2016

    KUBWA ZA USAJILI JUMAMOSI YA LEO HIZI HAPA

    Jamie Vardy 

    Vardy:Arsenal imeripotiwa kutegua kipengele cha mauzo kilichopo katika mkataba wa staa wa Leceister City Jamie Vardy kinachomruhusu mshambuliaji huyo mahiri kuondoka King Power kwa dau la £20m na tayari mazungumzo ya kutaka kumsajili yameshaanza.(The Guardian)

    Musona:Mshambuliaji wa FC Platinums ya Zimbabwe Walter Musona,21anatarajiwa kutua nchini leo kufanya mazungumzo ya mwisho na viongozi wa Yanga SC kabla ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.(Bingwa)

    Messi:Manchester United imedaiwa kuifuata Barcelona mara mbili katika kipindi cha wiki tatu zilizopita kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili staa wake Muargentina Lionel Messi hapo mwaka 2017.(Daily Mail)

    Wilshere:Baada ya kumnasa Ilkay Gundogan kocha wa Manchester City Muhispania Pep Guardiola ameripotiwa kuvutiwa na mpango wa kutaka kimsajili kiungo wa Arsenal Muingereza Jack Wilshere,23.(The Sun)

    Simeone:Diego Simeone amekataa ofa ya kujiunga na Paris Saint-Germain na badala yake ataendelea kubakia Atletico Madrid kwa msimu mwingine.(Gianluca di Marzio)

    Emery:Paris Saint-Germain imeripotiwa kumgeukia kocha wa Sevilla Unai Emery baada ya kugonga mwamba katika harakati zake za kumtaka kocha wa Atletico Madrid,Diego Simeone "El Cholo".( iTele)

    Amavi:Liverpool imeripotiwa kuvutiwa na mpango wa kutaka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Aston Villa,Jordan Amavi licha ya nyota huyo kutoonyesha kiwango bora msimu uliopita.Mbali ya Liverpool vilabu vingine vinavyomtaka Amavi ni AC Milan na Lyon.( L'Equipe)

    Pogba:Antonio Conte amewaambia mabosi wa Chelsea kutoa kitita cha €101m ili kumsajili kiungo wa Juventus Paul Labile Pogba kwani anatamani kufanya Kazi kwa mara nyingine na staa huyo wa Ufaransa.

    Bartra:Barcelona imetangaza kuwa imemuuza aliyekuwa mlinzi wake wa kati Marc Bartra kwenda Borussia Dortmund baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kukubali kutoa kitita cha €8m.Bartra,25,ameshinda vikombe 14 akiwa na Barcelona aliyojiunga nayo akiwa kinda wa miaka 12 tu.

    Koeman:Kocha wa Southampton Mholanzi Ronald Koeman ameuomba uongozi wa klabu hiyo umruhusu afanye mazungumzo na Everton ambayo siku za hivi karibuni imeripotiwa kuita saini yake.Wakati huohuo habari zinasema ikiwa Koeman ataondoka Southampton nyota watatu wa klabu hiyo Victor
    Wanyama, Shane Long na Graziano Pelle nao wataondoka. (Daily Express)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUBWA ZA USAJILI JUMAMOSI YA LEO HIZI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top