728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 09, 2016

    COPA AMERICA CENTENARIO:BRAZIL YAIFUNGA HAITI 7-1,ROBO FAINALI YANUKIA

    Orlando, Marekani.

    Brazil imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America Centenario baada ya kuichapa Haiti kwa mabao 7-1 katika mchezo wa Kundi B uliochezwa katika uwanja wa Orlanda Citrus Bowl,Orlando-Marekani.

    Mabao ya Brazil ambayo ilionekana kuwazidi karibu kila idara wapinzani wake Haiti yamefungwa na kiungo wake Phillipe Coutinho aliyefunga mabao matatu (hat trick) dakika za 14,29 na 90.

    Mabao mengine ya Brazil yamefungwa na Renato Augusto aliyefunga mara mbili dakika za 35 na 86,Lucas Lima dakika ya 67 na Gabriel Gabigol Barbosa dakika ya 59 huku lile la Haiti likifungwa na James Marcellin dakika ya 70.

    Kwa matokeo hayo sasa Brazil imefikisha pointi nne baada ya kucheza michezo miwili na inahitaji sare au ushindi wowote katika mchezo wake ujao dhidi ya Peru ili iweze kufuzu hatua ya robo fainali.Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumamosi Brazil ilitoka sare ya bila kufungana na Ecuador.

    VIKOSI

    Brazil: Allison, Dani Alves, Luis, Gil,Marquinhos, Willian, Augusto, Elias (Wallace 72'), Coutinho, Casemiro (Lucas Lima 62'),Jonas (Gabriel 46').

    Haiti: Placide, Jaggy,Goreux, Genevois,
    Alexandre (Hilaire 63'), Jerome, Lafrance,Alcenat (Maurice 82'), Marcelin, Belfort (Nazon 52'), Louis.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPA AMERICA CENTENARIO:BRAZIL YAIFUNGA HAITI 7-1,ROBO FAINALI YANUKIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top