728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 08, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI JIONI YA LEO JUNI 8,2016

    Vazquez

    Vazquez:Rais wa Palermo Maurizio Zamparini amekaririwa akisema kwamba Tottenham Hotspur wamewasiliana nae wakitaka kumsajili nyota wa klabu yake Franco Vazquez,27 ambaye msimu ulioisha wa Seria A alifanyiwa faulo mara 199. “Niko kwenye mazungumzo na Tottenham kuhusu Vazquez na nimewaambia watoe €25m (£19.6m) niwauzie.(Sky Sports)

    Morata:Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anataka kuwa na safu kali ya ushambuliaji msimu ujao na tayari amedaiwa kutaka kutoa kitita cha €60m ili kumsajili mshambuliaji wa Juventus Muhispania Alvaro Morata.Morata,23,ameifungia Juventus mabao 27 katika michezo 93 tangu alipojiunga nayo mwaka 2014 akitokea Real Madrid.(Marca)

    Coutinho:Liverpool imedaiwa kukataa ofa ya awali ya £23m toka Paris Saint-Germain kwa ajili ya kumuuza kiungo wake Mbrazil Philippe Coutinho. Coutinho,23,alijiunga na Liverpool mwaka 2013 akitokea Inter Milan kwa ada ya £8m.(Marca)

    Chong:Kinda wa Kidachi anayekipiga Feyenoord Tahith Chong amedokeza kuwa siku si nyingi atajiunga na Manchester United.Katika kuonyesha kuwa hatanii ,Ching,16,ameweka picha kwenye kurasa zake za instagram/twitter akiwa amevalia jezi ya Manchester United.(Daily Mail)

    Fligge:Afisa habari wa Borussia Dortmund amesema klabu hiyo haijafanya mawasiliano yoyote yale na Manchester City kuhusu kutakiwa kwa nyota wake Mgabon Pierre-Emerick Aubameyang,26, hivyo haina chochote cha kusema kwa sasa.(DPA)

    De Boer: Southampton imeripotiwa kuwa itajaribu kumshawishi Kocha wa zamani wa Ajax Frank De Boer kuwa kocha wake mpya pindi dili la kocha wake wa sasa Ronald Koeman kwenda Everton litakapokuwa limekamilika. (Daily Express)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI JIONI YA LEO JUNI 8,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top