California, Marekani.
TIMU ya Taifa ya Argentina imeanza vizuri kuusaka ubingwa wa kombe la Copa America Centenario baada ya kuinyuka timu ya taifa ya Chile kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa Kundi D ulioisha hivi punde huko katika dimba la Levi's Stadium,Santa Clara,California -Marekani.
Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kuisha bila ya timu yoyote kuuona mlango wa mwenzie,Argentina ilikianza kipindi cha pili kwa kasi na kandanda na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 51 kupitia kwa Angel Di Maria baada ya kumalizia kwa ustadi mkubwa pasi ya Ever Banega aliyewazidi maarifa walinzi wa Chile.
Dakika ya 59 Ever Banega aliandikia Argentina bao la pili baada ya kupokea pasi safi toka kwa Ever Banega na kufanya mchezo uishe kwa Argentina kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.Bao la Chile limefungwa dakika ya 93 na Jose Fuenzalida.
Katika mchezo mwingine wa Kundi D uliochezwa mapema huko katika dimba la Orlanda Citrus Bowl,Panama wameibuka wababe baada ya kuwafunga Bolivia kwa mabao 2-1.Mabao yote ya Panama yamefungwa na Blas Perez dakika za 11 na 87 huku lile la Bolivia likifungwa dakika ya 54 na Juan Arce.
Michuano hiyo utaendelea tena kesho Jumatano Juni 8 kwa michezo miwili ya Kundi A kuchezwa:Katika mchezo wa kwanza Marekani watacheza na Costa Rica na katika mchezo wa pili Colombia watavaana na Paraguay.
0 comments:
Post a Comment