728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 19, 2016

    SERENGETI BOYS YAENDELEA KUKOMAA INDIA,YATOKA 2-2 NA KOREA KUSINI

    Goa,India.

    TIMU ya soka ya Tanzania ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys leo jioni imeibana Korea Kusini na kutoka nayo sare ya mabao 2-2 katika mchezo mkali wa michuano maalumu ya vijana ya AIFF Youth Cup inayoendelea huko Tilak Goa,India. 

    Serengeti Boys ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa winga wake Asad Ali Juma.Asad alifunga bao hilo baada ya kuwalamba chenga walinzi watatu wa Korea Kusini.

    Baada ya bao hilo Korea Kusini walikuja juu wakiutumia vyema mfumo wao wa 4-2-3-1 na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 27 kupitia kwa kiungo wake Shin Sanghwi na kufanya timu zote ziende mapumziko zikiwa sare.

    Kipindi cha pili Korea Kusini ilikianza vyema baada ya kupata bao la kuongoza dakika ya 58 kupitia kwa Park Jeonghin.Park alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Joung Sungjune kuangushwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.

    Dakika ya 86 Mauli Lembe aliisawazishia bao Serengeti Boys na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya mabao 2-2.

    Katika michezo ya awali Serengeti Boys iliwafunga wenyeji India kwa mabao 3-1 kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na Marekani katika mchezo wa pili.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAENDELEA KUKOMAA INDIA,YATOKA 2-2 NA KOREA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top