Gent,Ubelgiji.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta leo ameshindwa kuipa ushindi timu yake ya KRC Genk baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na KAA Genk katika mchezo mkali wa mtoano wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Europa Ligi msimu ujao.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Ghelamco Arena huko Gent na kuchezeshwa na mwamuzi Bart Vertenten walinzi wa timu zote mbili walionyesha umakini mkubwa uliopelekea kutotoa mwanya kwa washambuliaji kufunga.
Dakika ya 61 KRC Genk iliamtoa Samatta na kumuingiza Neeskens Kebano lakini bado mabadiliko hayo hayakusaidia kwani KAA Gent ilionekana kujipanga vizuri zaidi.
Kwa sare hiyo ya leo KRC Genk sasa itabidi kushinda mchezo wake ujao dhidi ya mshindi kati ya Charleroi na Kortrijk ili ikate tiketi ya kucheza michuano ya Europa Ligi msimu ujao kupitia mtoano.
Matokeo mengine ya michezo ya leo yalikuwa hivi:
Club Brugge 2-2 KV Oostende
Anderlecht 2-0 SV Zulte Waregem
0 comments:
Post a Comment