728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, January 07, 2015

    NANI KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRICA HAPO KESHO?

    Lagos,Nigeria.

    Kesho tarehe 8 katika jiji la Lagos nchini Nigeria kazi itakuwa ni moja tu nayo si nyingine bali ni kumtangaza mchezaji bora wa mwaka wa Africa.

    Ufalme huo wa soka barani Africa unawaniwa na nyota Yaya Toure (Ivory Coast),Vincent Enyeama (Nigeria) na Aubameyang (Gabon).

    Wanaopigiwa upatu kuibuka na ushindi ni kiungo Yaya Toure na mlinda mlango Vincent Enyeama huku Aubameyang akiwa hapewi nafasi kubwa ya kuweka historia.

    Ikiwa Yaya Toure atatwaa ushindi katika mtifuano huo atakuwa ameweka historia ya kutwaa heshima hiyo kwa mara ya nne mfululizo.

    Vincent Enyama akitwaa ufalme huo atakuwa ni Mnigeria wa kwanza kufanya hivyo tangu Kanu Nwakwo alipofanya hivyo miaka 15 iliyopita.

    Nyota wa Nigeria waliowahi kutwaa ufalme huo ni Kanu Nwankwo,
    Victor Ikpeba, Emmanuel Amuneke na marehemu Rashidi Yekini.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NANI KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRICA HAPO KESHO? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top