Manchester,England.
Muda wowote kuanzia sasa klabu ya Manchester United itamtangaza mlinda mlango Victor Valdes 32 kuwa mchezaji wake mpya.
Valdes ambaye amekuwa hana timu kwa kipindi kirefu sasa tangu aachane na klabu yake ya Barcelona amekuwa akijifua na United kwa kipindi cha miezi miwili sasa huku akiendelea kupata matibabu ya jeraha lake la goti alilolipata mwaka jana.
Habari za kuamini toka ndani ya klabu ya Manchester zinasema kuwa Valdes anatarajiwa kusaini mkataba wa miezi 18 baada ya kumvutia kocha Louis Van Gaal.
Hata hivyo ujio wa Valdes aliyeichezea Barcelona michezo 535 na kutwaa mataji 6 ya La Liga na 3 ya ligi ya mabingwa ni habari mbaya kwa mlinda mlango Ben Amos ambaye ameambiwa atafute timu ya kwenda kuchezea.
0 comments:
Post a Comment