Mlinzi wa klabu ya Bayern Munich Mbrazil Dante amemuonya winga wa klabu hiyo Mjerumani Thomas Muller kuacha mara moja tabia ya kumtania vinginevyo atamdunda.
Dante ametamka hilo baada ya kuchoshwa na tabia ya Muller ambaye mara kwa mara amekuwa akimtania mlinzi huyo kwa kukumbushia ushindi wa mabao 7-0 iliyoupata timu yake ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia dhidi ya wenyeji Brazil ambao Dante alicheza.
Dante amesema yuko radhi kutaniwa utani wowote ule lakini siyo kukumbushwa kuhusu kipigo hicho ambacho kilileta simanzi na vilio katika nchi nzima ya Brazil.
0 comments:
Post a Comment