Madrid,Hispania.
Atletico Madrid imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Vicente Calderon baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Real Madrid katika mchezo wa hatua ya mtoano wa Copa del rey uliopigwa jana usiku.
Katika mchezo huo ambao wenyeji Atletico walimtumia kwa mara ya kwanza mshambuliaji wake mpya Fernando Torres ilijipatia goli lake la kwanza kupitia kiungo Raul Garcia dakika ya 58 kwa mkwaju wa penati kufuatia madhambi aliyofanyiwa na mlinzi wa Madrid Sergio Ramos.
Goli la pili la Atletico lilifungwa na mlinzi kinda wa klabu hiyo Mruguayi Jose Maria Gimenez na kuifanya Rojiblancos itoke kifua mbele kwa ushindi mnono wa goli 2-0.
Mchezo wa marudiano utapigwa wiki ijayo tarehe 15 huko Santiago Bernabeu nyumbani kwa Real Madrid.
Matokeo Mengine
Valencia 2-1 Espanyol
Villarreal 1-0 Sociedad
Ratiba ya Leo
Barcelona vs Elche (5:00 Usiku)
0 comments:
Post a Comment