728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 09, 2016

    AYEW ASAINI MIAKA MITATU WESTHAM NA KUWEKA REKODI YA USAJILI


    London,England.

    HATIMAYE nahodha msaidizi wa Ghana,Andre Ayew,ameihama Swansea City na kujiunga na West Ham United kwa dau la £20.5m na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa bei ya juu zaidi katika historia ya klabu hiyo ya jiji la London.




    Ayew,26,amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea Westham United na atakuwa akivalia jezi namba 20 badala ya namba 10 aliyokuwa akivaa Swansea City.

    Msimu uliopita Ayew aliifungia Swansea City mabao 12 katika michezo 34 aliyoanza katika kikosi cha kwanza cha kocha Francesco Guidolin.



    Ayew anaicha Swansea City ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu ajiunge nayo kwa uhamisho huru akitokea Olympique Marseille ya Ufaransa.

    Ayew anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Westham United katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Sofiane Feghouli,Havard Nordtveit,Toni Martinez na Arthur Masuaku.

    West Ham United iliyomaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita itafungua msimu mpya wkwa kuvaana na Chelsea siku ya Jumatatu usiku.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AYEW ASAINI MIAKA MITATU WESTHAM NA KUWEKA REKODI YA USAJILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top