728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 09, 2016

    NI UFUPI TU WA MATA AMA KUNA LINGINE ZAIDI?


    Na Chikoti Cico

    Baada ya klabu ya Manchester United kunyakua tuzo ya ngao ya jamii kwa kuifunga Leicester City kwa magoli 2-1, ushindi huo umegubikwa na picha mbaya ya kiungo wa klabu hiyo Juan Mata kuingizwa uwanjani dakika ya 63 ya mchezo na kutolewa dakika ya 90 ya mchezo. Tukio ambalo limevuta hisia za mashabiki na wachambuzi mbalimbali wa soka.

    Mata na Mourinho ambao wana historia mbaya kati yao hasa kwasababu wakati kiungo huyo alipokuwa anakipiga klabu ya Chelsea ni Mourinho huyo huyo aliyempakisha mabegi Mata na kumuuza kwa klabu ya Manchester United kwa kisingizio cha kwamba Mata “hafiti” kwenye mfumo wake, ya kwamba mchezaji huyo “hakabi ipasavyo”.

    Baada ya mchezo huo wa Ngao ya Jamii kuisha Mourinho alipoulizwa na waandishi wa habari kwanini alimtoa Mata, kocha huyo alisema “ ……Nilihitaji kumtoa mchezaji aliye mfupi zaidi kwasababu tulitarajia mipira mingi ya juu (kutoka kwa Leicester City) na Mata ni mchezaji mfupi ila nafikiri alicheza vizuri sana, alinipa kile ambacho nilihitaji, tulitaka kushinda na kila mmoja amefurahi mwishoni”.

    Ukiangalia sababu aliyoitoa Mourinho ni kweli ina mashiko kwa kiasi chake lakini kumwingiza Henrikh Mkhitaryan.ambaye urefu wake ni futi 5 na inchi10 huku Mata akiwa na urefu wa futi 5 na inchi7 hapo ndipo wasiwasi unapokuja kwamba inawezekana Mourinho alitaka KUMWELEZA kitu Mata.




    Pamoja na Mourinho kusema kwamba Mata yuko sawa kwa kitendo cha kutolewa baada ya kumwelewesha kwanini alimtoa lakini Mou anachosahau ni kwamba “MATENDO HUONGEA ZAIDI KULIKO MANENO” .

    Kitendo hicho ambacho mtangazaji wa BBC Danny Murphy amekisemea kwamba ni “kumwaibisha Mata mbele ya mashabiki wake na familia yake” kinatoa picha tata juu ya maisha ya kiungo huyo chini ya Mourinho hapo United.

    Swali la kujiuliza ni kwamba Mata yule aliyeondoshwa na Mourinho wakati akiwa Chelsea kwasababu ya “kutokukaba ipasavyo” amebadilika nini leo cha kuweza kumshawishi kocha huyo ambakishe na kumheshimu ndani ya United?

    Ukiachana na hali ya sintofahamu kati ya Mourinho na Mata pia usajili wa klabu ya Manchester unaonyesha dhahiri kwamba nafasi ya kiungo huyo itakuwa finyu mbele ya Mourinho hasa ukizingatia kwamba eneo la namba 10 ambalo Mata ni mjuzi tayari ameshabinafsishiwa Rooney ama Henrikh Mkhitaryan.

    Huku pia eneo la pembeni ambalo Mata anaweza kucheza kukiwa na wachezaji kama Rashford, Lingard, Martial na pia Mkhitaryan ama Young wachezaji ambao wanaweza kucheza eneo hilo hivyo kufanya maisha ya Mata pale United kuwa ya wasiwasi.

    Simtakii mabaya Mata chini ya kocha Jose Mourinho ila sitashangaa kwa mara ya pili kiungo huyo akikusanya kilicho chake na kutafuta maisha mengine nje ya Manchester United na kivuli cha hayo kutokea nafikiri ni tukio la kutolewa kwenye Ngao ya Jamii.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NI UFUPI TU WA MATA AMA KUNA LINGINE ZAIDI? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top