Manchester, England
SIYO TETESI TENA.Habari iko hivi.Klabu ya Manchester City imefanikiwa kukamilisha usajili mlinzi wa kimataifa wa England,John Stones,kwa ada ya uhamisho ya £47.5m ambayo baadae itapanda na kufikia £50m.
Stones,21,amesaini mkataba wa miaka sita wa kuitumikia miamba hiyo ya jiji la Manchester na atakuwa akivaliwa jezi namba 24.
Manchester City wamelazimika kuutangaza usajili huo kabla ya wakati waliopanga baada ya orodha ya kikosi chake kitakachovaana na Steaua
Bucharest siku ya Jumanne katika hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa Ulaya kuvuja katika mtandao wa UEFA kikiwa na jina la Stones na jezi namba 24.
Stones anakuwa mchezaji wa saba kujiunga na Manchester City katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya baada ya Ilkay Gundogan , Nolito , Oleksandr Zinchenko ,Aaron Mooy, Leroy Sane , Gabriel Jesus na Marlos Moreno.
Stones alijiunga na Everton mwaka 2013 akitokea Barnsley kwa ada ya uhamisho ya £3m.
0 comments:
Post a Comment