Baada ya nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kutangaza kuwa ataitema klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na hatimaye kuhitimisha safari ya miaka 17 ya kuitumikia miamba hiyo ya Anfield.
Siri imefichuka hasa juu ya kile kinachomuondoa klabuni hapo nyota huyo kipenzi cha mashabiki wa Liverpool.
Habari za kuaminika toka kwa Gerrard mwenyewe zinadai kuwa uchache wa mechi alizopaswa kucheza ndiyo sababu ya yeye kuamua kuondoka.
Gerrard anasema ``Brendan Rogers aliniita na kunikalisha chini na kisha kuniambia kuwa kwa sasa napaswa kuwa na idadi ndogo ya mechi ili kutoa nafasi kwa wenzangu.
Lilikuwa ni wazo zuri lakini kwa mtu ambaye umezoea kuanza katika kila mchezo niliona ni jambo gumu sana.Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nae.Naondoka kwa kuwa nahitaji muda mrefu zaidi wa kucheza.
Gerrard anatarajiwa kuhamia ligi ya Marekani huku timu inayohusiwa naye ikiwa ni Los Angels Galaxy kwa ofa ya paundi 3.5m.
0 comments:
Post a Comment