Barcelona,Hispania.
Goli la kujifunga la dakika ya pili la mlinzi wa Barcelona Jordi Alba lilitosha kuishushia timu hiyo kipigo cha kwanza cha mwaka 2015 toka kwa klabu ya Real Sociedad jana jumapili katika dimba la Anoeta.
Barcelona iliyoanza mchezo huo huku nyota wake Lionel Messi na Neymar wakiwa kwenye benchi ilishindwa kuipita ngome ngumu ya ulinzi ya Sociedad inayofundishwa na kocha David Moyes.
Kufuatia kipigo hicho Barcelona imeshindwa kuishusha kileleni klabu ya Real Madrid ambayo katika mchezo uliopigwa mapema katika dimba la Mestalla nyumbani kwa Valencia ilijikuta nayo ikiangukia pua baada ya kukubali kipicho cha goli 2-1.
Real ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata goli kupitia winga wake Cristian Ronaldo kwa mkwaju wa penati kabla ya Valencia kujibu kupitia kwa Antonio Garragan na mlinzi Nicolas Otamendi na kuzima ushindi wa Real wa mechi 22 mfululizo.
0 comments:
Post a Comment