728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 09, 2016

    ZAMALEK YAICHAPA AL AHLY NA KUTWAA UBINGWA WA "EGYPT CUP" KWA MARA YA 4 MFULULIZO


    Alexandria,Misri.

    MABAO mawili ya kipindi cha kwanza ya dakika za 20 na 24 ya Mshambuliaji,Bassem Morsi,yameiwezesha Zamalek kutwaa ubingwa wa nne mfululizo wa kombe la Misri maarufu kama Egypt Cup baada ya Jumatatu usiku kuwafunga wapinzani wao wakubwa Al Ahly kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Borg El-Arab huko Alexandria.

    Bao jingine la Zamalek katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi,Sandro Ando-Szabo kutoka nchini Hungary limetiwa kimiani na Mostafa Fathi katika dakika ya 59 ya kipindi cha pili huku lile la kufutia machozi kwa upande wa Al Ahly likifunga na Abdallah El-Said kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 33 ya mchezo.



    Aidha katika mchezo huo Al Ahly ililazimika kumaliza pungufu baada ya wachezaji wake wawili Hossam Ghaly na Ahmed Fathi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kuonyesha mchezo mbaya.

    Huo unakuwa ni ubingwa wa pili kwa Zamalek katika michuano hiyo kwani mwaka jana iliutwaa tena baada ya kuifunga Al Ahly kwa mabao 2-0 ya Bassem Morsi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ZAMALEK YAICHAPA AL AHLY NA KUTWAA UBINGWA WA "EGYPT CUP" KWA MARA YA 4 MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top