728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, January 11, 2015

    MKUDE FANYIA KAZI USHAURI WA PHIRI

    Na Paul Manjale.

    Hivi karibuni aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Mzambia Patrick Phiri alimshauri aliyekuwa kiungo wake Jonas Mkude afanye kila awezalo akacheze soka Ulaya.

    Phili amediriki kusema hayo baada ya kukoshwa vilivyo na kiwango safi cha kiungo huyu mkabaji wa Simba.Ambaye baadhi ya mashabiki wamejaribu kwenda mbali na hata kumfananisha na Cob Web (Utando wa Buibui) kwa jinsi alivyo mahiri katika kuilinda klabu yake dhidi ya mashambulizi toka kwa klabu pinzani.

    Kwa mujibu wa Mkude mwenyewe anasema ilikuwa ni kawaida kwa kocha Phiri kumpigia simu na kumualika nyumbani kwake.Huko walikuwa wakiongea mengi yahusuyo mpira huku mara kwa mara akimshauri akacheze soka Ulaya na kumtaka apunguze mizaha uwanjani na kuzidisha bidii mazoezini.

    Phiri ni sehemu tu kati ya wadau wengi ambao tunataka kuona wachezaji wetu wakipata nafasi ya kusakata soka la kulipwa barani Ulaya.

    Kucheza soka Ulaya kuna raha yake na faida zake.Kwani licha ya kumfaidisha  mchezaji husika pia hulifaidisha hata taifa analotokea.

    Tazama kucheza soka England kwa Paul Wanchope kulivyofungua milango kwa kizazi cha akina Joel Campbell na wenzie.

    Ni klabu ipi leo hii ingeitupia jicho Costa Rica nchi ndogo masikini yenye wakazi wasiozidi milioni nne kama kusingekuwepo na sababu ya kufanya hivyo?

    Wachezaji wetu wanapaswa kupokea ushauri wanaopewa na kuufanyia kazi.Wajifunze kupitia wenzao wa Kenya na Uganda ambao soka la ndani kwao siyo kipaumbele tena.

    Hawazitazami tena Gor Mahia,Fc Leopards,Ura ama  Sports Club Villa kwa jicho lile lile la mwaka arobaini na saba.Wanazitazama kwa jicho jipya,jicho la ngoja twende tutarudi baadae.Wameisikia sauti iliayo nyikani na kuifuata.

    Unadhani Victor Wanyama angefika Ulaya kama asingeuchukua ushauri wa kaka yake MacDonald Maliga na kuufanyia kazi?Thubutu!!

    Je,nini kingejiri kama angetia pamba masikioni mwake? Siyo ajabu mpaka leo hii angekuwa anasukuma siku pale Sofapaka na huenda siku moja angekuja Yanga au Simba na kuondoka bila kuaga kama wenzie akina Mark Silengo na Joseph Shikokoti.

    Huu ni ushauri ambao Jonas Mkude na kambi yake hapaswi kuulazia damu hata kidogo.Wazungu wanasema hivi Now or Never yaani Sasa au Hapana.Akili kumkichwa

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MKUDE FANYIA KAZI USHAURI WA PHIRI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top