728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 14, 2017

    Serengeti Boys yapata pigo,Nahodha wake avunjika mguu


    Gentil,Gabon.

    TIMU ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17,Serengeti Boys ambayo kesho Jumatatu itaanza kutupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya vijana ya AFCON huko nchini Gabon kwa kuvaana na vijana wenzao wa Mali imepata pigo baada ya Nahodha Issa Abdi Makamba kuvunjika mguu.

    Kocha Mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime 'Mchawi Mweusi' amesema Issa amepata mpasuko kwenye mguu wake wake wa kulia na atakosa michezo yote ya michuano hiyo.

    Wakati huohuo Shime ameongeza kuwa tayari ameshawapanga vyema vijana wake kuziba nafasi ya Issa.Pia Shime amewataka Watanzania kuiombea timu hiyo ili iweze kufanya vyema kwenye michuano hiyo ambayo imeanza leo.

    Serengeti Boys itashuka dimbani kesho Jumatatu kucheza na Mali ambao ni mabingwa watetezi wa michuano ya vijana.Mchezo huo utaanza mishale ya saa 9:30 za Gabon ambazo ni saa 11:30 jioni kwa saa za Tanzania.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Serengeti Boys yapata pigo,Nahodha wake avunjika mguu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top