728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 14, 2017

    AFCON U-17:Wenyeji Gabon washushiwa kichapo cha Mbwa Mwizi

    Gentil,Gabon.
    MICHUANO ya Afrika ya vijana wenye umri wa miaka 17 imeanza kutimua vumbi lake leo Jumapili kwa wenyeji Gabon kuanza kinyonge kutupa karata zake baada ya jioni ya leo kukubali kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa vijana wenzao wa Guinea kwenye mchezo wa kwanza wa kundi A uliochezwa kwenye uwanja wa Stade Port-Gentil.
    Guinea waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa Fandje Toure.Dakika 15 baadae Elhadj Abourahmane Bah aliifungia Guinea bao la pili.
    Katika dakika ya 30 Elhadj Abourahmane Bah aliifungia Guinea bao la tatu kabla ya Aguibou Camara kufunga bao la nne na kufanya vijana hao waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 4-0.
    Kipindi cha pili walikuwa ni Guinea tena walioendelea kutakata baada ya kufunga bao la tano kupitia kwa Fandje Toure kabla ya wenyeji Gabon kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Richard Ndzengue katika dakika ya 70 ya mchezo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AFCON U-17:Wenyeji Gabon washushiwa kichapo cha Mbwa Mwizi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top