Lubumbashi,Congo.
TP Mazembe imeanza vyema
kuutetea ubingwa wake wa kombe la shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo kuitambia
CF Mounana ya Gabon kwa kuifunga mabao 2-0 kwenyemchezo wa kwanza wa kundi D uliochezwa
kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe huko Lubumbashi.
Ushindi huo
umeipeleka TP Mazembe kileleni mwa msimamo wa kundi D baada ya kufikisha pointi
tatu kufuatia kushuka dimbani mara moja. CF Mounana inashika mkia kwenye kundi
hilo.
Ilimchukua dakika 18 Tresor Mputu Mabi kuifungia TP Mazembe bao la
kuongoza akitumia vyema pasi ya. Issama Mpeko.Bao
hilo lilidumu mpaka mapumziko. Kipindi cha pili nahodha Rainford Kalaba aliipa
TP Mazembe uhakika wa kuibuka na pointi tatu baada ya kufunga bao la pili baada
ya kazi nzuri ya Mazembe Solomon Asante
0 comments:
Post a Comment