Gentil, Gabon.
TIMU ya taifa ya Ghana,Black Starlets imeianza michuano ya AFCON ya vijana kwa staili yake baada ya Jumapili usiku kuishushia kichapo cha Mbwa Mwizi Cameroon kwa kuifumua mabao 4-0 kwenye mchezo wa pili wa kundi A uliochezwa huko Stade Port Gentil.
Iliwachukua Ghana dakika 25 tu kufunga bao la kwanza kupitia kwa nahodha wake Eric Ayiah.Dakika ya 32 Ibrahim Sulley aliifungia Ghana bao la pili kabla ya kufunga la tatu dakika mbili baadae na kufanya vijana hao waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili walikuwa ni Ghana tena waliondelea kuwanyanyasa wapinzani wao kwa kuongeza bao la nne katika dakika ya 64 kupitia kwa nahodha wake Eric Ayiah.
Katika mchezo mwingine wa kundi A,wenyeji Gabon walikutana na kipigo kikali cha mabao 5-1 kutoka kwa Guinea.
Leo Jumatatatu michezo ya kundi B itachezwa ambapo katika mchezo wa kwanza utakaochezwa saa 11:30 jioni za Tanzania,Serengeti Boys itashuka dimbani kucheza na mabingwa watetezi Mali.
0 comments:
Post a Comment