Mouscron,Ubelgiji.
KRC Genk ya Mtanzania,Mbwana Ally Samatta imeendelea kujikusanyia pointi za kutosha kwenye kundi lake la A baada ya usiku wa kuamkia leo ikiwa ugenini kuwatwanga wenyeji wao Royal Excel Mouscron mabao 2-0 huko Stade Le Canonnier ikiwa ni katika muendelezo wa michezo ya kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Europa Ligi msimu ujao.
Katika mchezo huo ulioshuhudiwa Samatta akicheza dakika zote tisini,Genk ilijipatia mabao yote mawili katika kipindi cha pili kupitia kwa Ruslan Malinovsky aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 63 na Jean-Paul Boëtius aliyefunga bao la pili katika dakika ya 70.
Ushindi huo umeifanya Genk iendelee kujitanua kileleni mwa kundi A baada ya kuvuna pointi 22 katika michezo yake minane.Royal Excel Mouscron iko nafasi ya sita ikiwa na pointi nane baada ya michezo minane.Genk tayari imeshafuzu Europa Ligi.
0 comments:
Post a Comment