Libreville,Gabon.
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 17,Serengeti Boys imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga nusu fainali ya michuano ya AFCON ya vijana baada ya jioni ya leo kupata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano kwa kuwafunga vijana wenzao wa Angola mabao 2-1 katika mchezo wa kundi B uliochezwa huko Libreville,Gabon.
Ikicheza kandanda safi na la kuvutia iliwachukua Serengeti Boys dakika 6 tu kuandika bao lake la kwanza kupitia kwa kiungo wake,Kelvin Nashoni Naftal aliyefunga kwa kichwa akiunganisha kona fupi kutoka kulia mwa uwanja.
Katika dakika ya 69 Abdul Hamis Selemani aliihakikishia Serengeti Boys pointi zote tatu baada ya kufunga bao la pili kwa shuti Kali.Bao la Angola limefungwa na Pedro Domingos Costinho katika dakika ya 19 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Orando.
Ushindi huo umeifanya Serengeti Boys ikae kileleni mwa msimamo wa kundi A baada ya kufikisha pointi nne katika michezo miwili iliyocheza mpaka sasa.
Sasa Serengeti Boys inahitaji kushinda ama kutoka sare mchezo wake wa Jumapili dhidi ya Niger ili iweze kujihajikishia nafasi ya kufuzu nusu fainali ya AFCON pamoja na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment