Paris,Ufaransa.
KARIM Benzema ameendelea kususwa/kuwekewa ngumu kurejea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa baada ya leo hii jina lake kutotajwa kwa mara nyingine kwenye kikosi cha wachezaji 26 ambacho mwezi ujao kitacheza michezo mitatu ya kimataifa dhidi ya Paraguay,England na Sweden.
Staa huyo wa Real Madrid aliingia matatizoni mwaka juzi na kuondolewa kwenye kikosi cha kocha Didier Deschamps akituhumiwa kutaka kujaribu kujipatia pesa kiudanganyifu kupitia kashfa ya mkanda wa ngono unaomhusisha staa wa Olympique Marseille,Mathew Valbuena ambaye naye aliondolewa kikosini.
Benzema hajaichezea Ufaransa tangu Octoba 2015 alipoifungia timu hiyo mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Armenia.
Alexandre Lacazette
Wakati Benzema akitoswa staa wa Lyon, Alexandre Lacazette yeye amekumbukwa baada ya kuwa nje ya kikosi cha Ufaransa kwa kipindi kirefu.
Mwingine aliyekumbukwa ni beki kati wa Chelsea,Kurt Zouma ambaye licha ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani mwaka mzima lakini jicho la Deschamps limemuona.
Kikosi Kamili cha Ufaransa ambacho kimetangazwa na Kocha,Deschamps ni pamoja na
Makipa:Alphonse Areola (Paris Saint-Germain), Benoit Costil (Rennes), Hugo Lloris (Tottenham)
Mabeki:Lucas Digne (Barcelona),Christophe Jallet (Lyon), Presnel Kimpembe (Paris Saint-Germain), Laurent Koscielny (Arsenal), Benjamin Mendy (Monaco), Djibril Sidibe (Monaco), Samuel Umtiti (Barcelona),
Raphael Varane (Real Madrid), Kurt Zouma (Chelsea)
Viungo:N'Golo Kante (Chelsea), Blaise Matuidi (Paris Saint-Germain), Paul Pogba (Manchester United), Adrien Rabiot (Paris Saint-Germain), Moussa Sissoko (Tottenham),Corentin Tolisso (Lyon)
Washambuliaji:Ousmane Dembele (Borussia Dortmund), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Alexandre Lacazette (Lyon), Thomas Lemar (Monaco),Kylian Mbappe (Monaco), Dimitri Payet (Marseille), Florian Thauvin (Marseille)m
0 comments:
Post a Comment